KITI KILICHOKUWA WAZI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Kiti Kilichokuwa Kimeachwa Wazi

Kila siku wakati wa mapumziko watoto wengi walikimbilia uwanjani. Lakini kwenye kona moja ya uwanja kulikuwa na kiti ambacho mara nyingi kilibaki wazi.

Siku moja mtoto mpya alikuja shuleni. Hakumjua mtu yeyote. Alisimama karibu na uwanja akiwa ameshika chupa yake ya maji akiwatazama wenzake wakicheza.

Hakujua aanzie wapi. Muda wa mapumziko ulipomalizika alirudi darasani na kukaa kimya.

Kesho yake jambo lile lile lilitokea.


Siku ya tatu mtoto mmoja alipita karibu na kile kiti kilichokuwa wazi. Alisimama kwa muda akamtazama yule mtoto mpya kisha akakaa pembeni yake.

Hakukuwa na maneno mengi Alimpa tu nafasi ya kukaa pamoja naye.

Siku zilizofuata watoto wengine nao walianza kumkaribia. Hatimaye yule mtoto mpya alianza kucheza, kucheka na kushiriki katika shughuli za darasani.

Baada ya wiki kadhaa kiti kile kilibaki wazi tena.

Lakini safari hii si kwa sababu mtoto alikuwa peke yake.

Kilikuwa wazi kwa ajili ya mtoto mwingine ambaye angehitaji mtu wa kumkaribisha.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments