Katuni zageuka tishio kwa mtoto


Timothy Lugembe,

Mwanakwetukids.

Hapo mwanzo maudhui ya katuni yalianzishwa kwa lengo la kufurahisha na kuburudisha, lakini kwa watoto zilitumika kama sehemu ya kufurahi na kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo michezo , kuongea, na mambo ya kitaaluma ikiwemo kuhesabu na kuongea.

Televisheni kupitia visimbuzi mbali mbali, vimeveba channeli tofauti tofauti zenye maudhui ya katuni kwaajili ya watoto kujifunza na kufurahia wanapokuwa majumbani. Wazazi wengi huamini kuwa katuni ni kitu Bora na salama kwa mtoto kuangalia kuliko vipindi vingine , kitu ambacho kwa ulimwengu wa sasa sio sahihi.

Kwa kuzingatia nadharia ya Cultivation iliyo asisiwa na George Gabner 1960, nadharia inaleza kuwa.

"Kadri mtu anavyotumia muda mwingi kwenye vyombo vya habari/televisheni hasa anapotazama maudhui yanayo jirudia, ndivyo anavyoweza kuanza kuaminika kwamba Dunia halisi ndivyo ipo kama inavyo onekana kwenye vyombo hivyo".

Kwa sasa Kuna maingizo ya katuni zenye maudhui mabaya yanayo lenga kuharibu mtoto ama kumuingizia kitu kipya kisicho sahihi kwenye ubongo wake "USHOGA". Baadhi ya maudhui yamekuwa yakionyesha tabia ambazo ni hatarishi kwa mtoto , mfano katuni wa kiume wakibusiana , wakilishana, wakijiremba, wakivalia mavazi ya kike, wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na tabia nyingine nyingi zenye dalili za mapenzi ya jinsia Moja hivyo hivyo kwa katuni wakike.

Kwa mtoto kuangalia vitendo hivyo mara kwa mara kunamfanya aamini kuwa vitu vinavyo fanyika kwenye katuni ndivyo vilivyo na hakuna ubaya na wao wakifanya. Hapo ndipo mzazi ataanza kumuona mtoto anakuwa na tabia ambazo sio za kawaida kutokana na mafunzo aliyo yapata kwenye katuni 


Watoto wanatabia ya kushiriki na kufundishana tabia mbali mbali wanapokutana pamoja , pindi wanapokuwa mashuleni mtoto alieiga tabia mbaya kutoka kwa katuni ataona ni kawaida kufanya vitendo hivyo akiwa na wenzake na wenzake wakafanya kwa wenzao na mwisho wa siku kunasababisha uharibifu wa watoto, na mafunzo hayo yanaweza kufanyika kwenye mazingira yanayo wakutanisha watoto pamoja mfano mashuleni.

Maudhui hayo hayatengenezwi kwa bahati mbaya bali ni mkakati wa Siri unaofanyiwa kazi na upande wa GIZA kuhakikisha idadi ya watu inapungua ulimwenguni, na Kwa kutekeleza hili ni lazima watoto waharibiwe kwa kuingiziwa kumbu kumbu chafu kwa kutumia maudhui ambayo yanaonekana ni salama kwao.

Kwa wazazi na walezi na waalimu mashuleni ni jukumu lao kuwa makini na kufuatili mienendo ya watoto muda wote kwa kuzingatia kuwa Dunia ya sasa sio mahali salama. Kabla ya mtoto kuanzia kuangalia chochote ni muhimu mzazi au mlezi kuhakikisha anajiridhisha na maudhui hayo kabla ya kumfikia mtoto. Kwa waalimu mashuleni ni wajibu wao kukemea vitendo au viashiria vya uharibifu ambavyo vinaweza kuonekana miongoni mwa watoto.

Kama taifa tunaweza kutengeneza katuni wetu wenyewe ambao watamfundisha mtoto maadili mema ikiwemo kuanzisha vita dhidi ya mambo machafu nchini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments