FANYA MEMA HATA KAMA HAKUNA ANAYEKUONA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Asubuhi ya Jumatatu ilianza kama siku nyingine. Wanafunzi walikuwa wakielekea madarasani, walimu wakijiandaa kufundisha na uwanja wa shule ulijaa sauti za watoto wakicheka.

Amani mwanafunzi wa darasa la saba alipofika darasani alikuta bahasha ndogo juu ya dawati lake. Juu yake kulikuwa na maandishi.

Alifungua bahasha kwa hamu. Ndani kulikuwa na barua iliyosema

"Nimekuwa nikikuona ukiwasaidia wanafunzi wapya bila kutarajia malipo wala sifa. Asante kwa kuwa mfano mzuri"

Hakukuwa na jina la aliyeandika.

Siku nzima Amani alijiuliza ni nani aliyekuwa ametuma barua hiyo. Alipowauliza marafiki zake wote walitikisa vichwa wakisema hawajui.

Wiki moja baadaye.wakati wa mkutano wa shule mwalimu mkuu alisema "Wakati mwingine wema hufanywa kimya kimya lakini huwa unaonekana"

Kisha akamwita Amani mbele ya wanafunzi wote na kumkabidhi cheti cha Mwanafunzi Mwenye Maadili Bora. Ilibainika kuwa walimu walikuwa wakifuatilia tabia za wanafunzi kwa muda mrefu na mmoja wao ndiye aliyemwandikia ile barua ili kumtia moyo.

Amani alitabasamu. Aligundua kwamba kufanya jambo jema hakuhitaji kushuhudiwa na kila mtu. Wema hujenga heshima na huwagusa watu kwa njia ambazo wakati mwingine hatuzioni.




emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872



0/Post a Comment/Comments