BRIGHT ANAJIFUNZA UMUHIMU WA KUNYWA DAWA


EmakulataMsafiri

Mwanakwetukids

Bright ni mtoto mwenye tabia nzuri, mtiifu na anayependa kucheza na marafiki zake. Wazazi wake wanampenda sana kwa sababu ni mwenye heshima na anapenda kujifunza. Hata hivyo Bright ana changamoto moja kubwa hapendi kunywa dawa. Kila anapopewa dawa hulia hukataa kufungua mdomo au hujificha ili asizinywe.

Siku moja Bright alipata homa kali na kukohoa. Mama yake alimpeleka hospitalini ambako daktari alimchunguza na kumpa dawa za kutumia kwa siku kadhaa. Waliporudi nyumbani ulifika muda wa kunywa dawa.

Mama: Bright muda wa kunywa dawa umefika.

Bright: Hapana mama sitaki dawa ni chungu sana.

Mama: Najua si tamu lakini dawa zitakusaidia kupona. Ukizikataa ugonjwa unaweza kuchelewa kuisha.

Bright: Lakini siwezi kuvumilia ladha yake.

Mama: Hebu tufikirie unapenda kucheza mpira, kukimbia na kucheza na marafiki zako sivyo?

Bright: Ndiyo napenda sana.

Mama: Ili urudi kufanya hayo yote mwili wako unahitaji kupona. Dawa ni kama mashujaa wanaoingia mwilini kupambana na vijidudu vinavyokusababishia ugonjwa.

Wakati huo Bright anakumbuka maneno ya daktari.

Bright: Sawa mama nitakunywa dawa. Nataka nipone haraka nirudi kucheza.

Mama anatabasamu anamsaidia Bright kunywa dawa kisha anampa maji.

Mama: Hongera sana Bright! Umefanya uamuzi mzuri. Ukiendelea kunywa dawa kama ulivyoelekezwa utapona haraka.

Bright: Kuanzia leo sitakuwa naogopa dawa. Najua zinanisaidia kuwa na afya njema.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872




0/Post a Comment/Comments