Watanzania Wengi Wanapata Huduma Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

 

 



Adeladius Makwega

Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa – DODOMA

 

“Kazi ya idara hii ninayoiongoza ni kukusanya nyaraka mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi, kigezo kikubwa kikiwa ni kwamba nyaraka hizo ziwe na umuhimu mkubwa kitaifa hivi karibuni tumewafikia watu binafsi. Hivi karibuni tumehifadhi nyaraka kutoka kwa Kanyama Chiume, Shaaban Robert na wengineo.

 

Pia, jukumu lingine ni kuhudumia watafiti wa ndani na nje ya nchi, kufanyia ukarabati wa nyaraka hizo na, mwisho, kuuhabarisha umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi nyaraka hizo.”

 

Mkurugenzi Kolokota aliongeza kuwa:

 

“Hapa tuna nyaraka za tangu enzi za Mjerumani, Mwingereza na hata za sasa.”

 

Ndugu Kolokota aligonga msumari wa mwisho wa nyaraka kwa kusema:

 

“Kwa zamani, idara yetu ilikuwa inapokea watafiti wengi kutoka nje ya nchi, lakini sasa watafiti wa ndani wamekuwa wengi zaidi kutokana na uelewa kuwa mkubwa kwa Watanzania. Hivyo, nahimiza kila mmoja wetu atunze nyaraka hizo, na idara yetu ni yetu sote.”

Haya ni matukio ya Agosti 19, 2026, ambapo Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kilikusanya taarifa hizi baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Huduma za Nyaraka kutoka Ofisi ya Rais, Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, ndugu Athanas Bernad Kolokota.

 

Safari ya kigulu  na njia ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha taasisi hii ya umma kilifika kwa Mkuu wa Huduma za Kumbukumbu, ndugu Emilios Muungano. Yeye alisema:

 

“Huduma zetu hutolewa baada ya kila mtafiti kutoka nje ya nchi kupitia COSTECH, kisha kufika hapa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Hapo hapo COSTECH hulipa, na baadaye mtafiti nakuja kwetu na hupewa huduma yetu. Hii ni kwa wageni, lakini kwa sisi Watanzania huduma hii hutolewa bure wanapokuwa na barua za utambulisho au vitambulisho kama vile NIDA, na huwa hawalipi gharama yoyote ile.”

 

Huu ni muhtasari wa matukio yaliyokusanywa Agosti 19, 2026, hapa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Kumbuka:

 

“Watanzania Wengi Wanapata Huduma Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.”

 

Nakutakia siku njema.


makwadeladius@gmail.com
0717649257

 








 

 

0/Post a Comment/Comments