USIAMINI UVUMI BILA KUTAFUTA UKWELI


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Kila jioni sauti ya mtu akiimba ilisikika kutoka nyumba moja iliyokuwa mwisho wa mtaa. Watu wengi walivutiwa na sauti hiyo tamu lakini hakuna aliyewahi kumwona mwimbaji. Dirisha lilikuwa limefungwa kila wakati.

Watoto wa mtaa walijenga hadithi nyingi. Wengine walisema alikuwa msanii maarufu aliyejificha. Wengine walidai huenda alikuwa mzee tajiri asiyeonekana hadharani.

Siku moja umeme ulikatika. Nyimbo hazikusikika tena. Watoto wakaamua kubisha hodi ili kujua kilichotokea.

Mlango ulipofunguliwa walimkuta bibi mmoja akiwa amekaa kwenye kiti. Alikuwa na redio ndogo mezani na kitabu cha nyimbo mikononi. Akacheka na kusema "Nyimbo mlizokuwa mnasikia si zangu. Nilikuwa naimba pamoja na redio kila jioni leo betri zimeisha"

Watoto wote walitabasamu walikuwa wameamini mambo mengi bila kujua ukweli.

Tangu siku hiyo kila Jumamosi walimtembelea bibi huyo. Waliimba naye, wakamsaidia kufanya usafi wa nyumba na walijifunza nyimbo nyingi mpya.



emakulatemsafiri@gmail.com 


0653903872

0/Post a Comment/Comments