Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Amina ambaye aliishi na wazazi wake pamoja na kaka yake Juma. Amina na Juma walipendana sana na walikuwa wakisaidiana kila siku.
Siku moja Juma aliugua na hakuweza kwenda shule. Amina alimuandalia uji, akamuandikia maswali ya darasani na kila mara alimhimiza kwa maneno ya upendo.
Baada ya siku chache Juma alipona. Alimshukuru Amina kwa kumjali na kusema "Dada yangu upendo wako umenifanya nijisikie mwenye nguvu na furaha".
Wazazi wao walifurahi kuona watoto wao wakipendana na kusaidiana. Waliwaambia familia yenye upendo huwa na furaha na umoja"
Kuanzia siku hiyo,Amina na Juma waliendelea kuishi kwa upendo kuheshimiana na kuwasaidia wengine waliokuwa na uhitaji.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872️


Post a Comment