Adeladius Makwega
Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa – DODOMA
Mafanikio ya taasisi hayajengwi na jina la taasisi pekee, bali na watu wanaoitumikia. Huo ndio ujumbe wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bi. Salama Said Mohammed, kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Akizungumza na baadhi ya watumishi jijini Dodoma Agosti 17, 2026, Bi. Salama aliwataka watumishi kufanya kazi kwa bidii, umahiri na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya taasisi.
“Unachopaswa kufanya unapofika katika taasisi ni kuangalia mpango kazi wa taasisi, kisha uangalie kile unachopaswa kufanya kwa kuzingatia miongozo ya taasisi, kanuni na sheria. Kisha fanya kazi kwa juhudi na kujituma ili kuhakikisha taasisi yako inasonga mbele,” alisema.
Bi. Salama alisisitiza kuwa utumishi wa umma ni dhamana, hivyo kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi bila kuchoka ili kuwatumikia wananchi wa Tanzania.
Kwa mtazamo wake, mtumishi mmoja anaweza kuwa sehemu ya mafanikio au changamoto ya taasisi. Anapowajibika, taasisi inasonga mbele; na taasisi inapofanya vizuri, wananchi ndio wanaonufaika.
Ndiyo maana kila mtumishi anapaswa kuwa “taa inayong’aa” ndani ya taasisi yake kwa kutimiza wajibu wake kwa uadilifu, bidii na kujituma.
Na muhimu zaidi, ujumbe huu unatoka kwa Bi. Salama Said Mohammed wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa—si Salama Binti Jabir.
Mwanakwetu, upo?
Kumbuka:
“Ujumbe wa Salama wa Kumbukumbu na Nyaraka.”
makwadeladius@gmail.com
| 0717649257
.gif)
Post a Comment