UAMINIFU NI HAZINA ISIYOFUTIKA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Neema alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano aliyeishi mjini. Alikuwa na mkoba wa bluu alioupenda sana kwa sababu ulikuwa zawadi kutoka kwa bibi yake.

Siku moja baada ya kutoka shule alipanda daladala kuelekea nyumbani. Aliposhuka aligundua kuwa alikuwa ameusahau mkoba wake kwenye siti ya basi.

Moyo wake ulianza kwenda mbio. Ndani ya mkoba kulikuwa na vitabu, daftari na kazi ya mradi aliyokuwa ameifanyia kazi kwa wiki nzima.

Yeye na baba yake walirudi haraka kwenye kituo cha daladala kuulizia lakini basi lilikuwa tayari limeondoka.

Kesho yake asubuhi walikwenda tena kituoni. Kondakta mmoja aliwaona na kuuliza Je mlikuwa mnatafuta mkoba wa bluu?


Neema akatikisa kichwa kwa furaha kondakta alimkabidhi mkoba huo baada ya abiria wote kushuka dereva aliuona chini ya kiti. Neema alifungua mkoba kila kitu kilikuwa salama.

"Asante sana" alisema kwa tabasamu.

Dereva akasema "Vitu vinaweza kununuliwa tena lakini uaminifu hauwezi kununuliwa"

Kuanzia siku hiyo Neema alianza kuandika jina na namba ya simu ya mzazi wake kwenye vitu vyake muhim na kila alipopanda daladala alihakikisha hakusahau chochote.



emakulatemsafiri@gmail.c

om 

0653903872

0/Post a Comment/Comments