UAMINIFU NA BUSARA HUENDANA PAMOJA

 


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Ilikuwa Jumamosi asubuhi. Ethan aliandamana na mama yake kwenda bustani ya mjini. Wakati mama yake alipokuwa akinunua maji Ethan aliketi kwenye benchi akisubiri.

Ghafla aliona pochi ndogo ya kahawia chini ya benchi.

Aliichukua na kuifungua kidogo. Ndani kulikuwa na kitambulisho, kadi za benki na kiasi kidogo cha fedha. Ethan alitaka kumpelekea mama yake lakini kabla hajafika alimuona mzee mmoja akizunguka huku akiangalia chini kwa wasiwasi.

Ethan akamsogelea. "Samahani umepoteza kitu"?

Mzee akasema kwa sauti ya huzuni "Nimepoteza pochi yangu ilikuwa na kadi zangu zote humo".

Ethan hakumkabidhi mara moja. Akauliza "Pochi yako ina rangi gani? Na ndani kuna nini mbali na vitambulisho"?

Mzee akajibu kwa usahihi. Ethan akatabasamu na kumpa pochi yake.

Mzee alipumua kwa afueni.

"Asante sana mwanangu leo usingeirudisha ningepata shida kubwa"

Mama yake Ethan alisikia mazungumzo hayo na akampongeza.

Aliporudi nyumbani Ethan aligundua kuwa kufanya jambo sahihi hakuhitaji mtu akuone. Kilichokuwa muhimu ni kujua kwamba alikuwa amemsaidia mtu aliyekuwa na uhitaji.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments