SIMU ILIYOPIGA MARA MOJA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Kevin alikuwa mtoto wa darasa la sita aliyeishi mjini. Kila jioni alipenda kumsaidia mama yake katika duka dogo la vifaa vya shule.

Siku moja walipokuwa wakifunga duka simu ya mezani ililia mara moja tu kisha ikakata. Baada ya dakika chache ikalia tena na kukatika.

Kevin alishangaa.Kesho yake jambo lile lilijirudia akaamua kukaa karibu na simu ili ajibu haraka.

Ilipolia aliipokea "Halo?"

Sauti ya msichana mdogo ilisikika kwa aibu.

"Samahani... nilikuwa nataka kujua kama duka lenu linauza madaftari".

Kevin akamuuliza kwa nini ulipiga na kukata mara mbili.

Msichana akajibu "Nilikuwa na vocha ndogo sana niliogopa zingeisha kabla sijazungumza".

Kevin alimwambia "Usijali njoo kesho asubuhi tutakuwekea daftari.

Asubuhi yake msichana alifika akiwa na fedha za kununua daftari. Kevin alimkabidhi daftari na kalamu moja ya zawadi.

Wiki chache baadaye msichana huyo alirudi dukani akiwa na cheti cha ufaulu.

Kevin alitabasamu. Aligundua kuwa wakati mwingine msaada mdogo unaweza kuwa mwanzo wa mafanikio makubwa ya mtu mwingine.



emakulatemsafiri@gma

il.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments