SI KILA WAZO ZURI NI RAHISI KUTEKELEZWA



Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Hapo zamani panya wengi waliishi kwenye ghala la nafaka. Lakini kulikuwa na paka mjanja aliyewavizia kila siku.

Siku moja panya wakafanya mkutano Panya mmoja mdogo akasema "Tufunge kengele shingoni mwa paka. Kila atakapokuja kengele italia na tutakimbia"

Panya wote wakapiga makofi na kusema "Hilo ni wazo zuri sana"

Lakini panya mzee akainuka na kuuliza "Ni nani atakayemfunga paka kengele"?


Ukumbi ukawa kimya. Hakuna panya aliyethubutu kujitolea.

Hapo ndipo walitambua kuwa wazo zuri ni jambo moja lakini kulitekeleza ni jambo lingine.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872

0/Post a Comment/Comments