.gif)
Adeladius Makwega – Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka – DODOMA
Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa imeendelea na shughuli zake jijini Dodoma, ambapo Agosti 18, 2026, kumefanyika vikao kadhaa vya ndani. Kikao kikubwa kilikuwa kile cha Kamati ya Ukaguzi cha Robo ya Nne ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika Agosti 18, 2026.
Kikao hiki kimefanyika vizuri chini ya ajenda sita, huku kikiwa na ajenda mama mbili, yaani yatokanayo na kikao cha Robo ya Tatu ya mwaka wa 2025/2026 na taarifa ya ukaguzi ya Robo ya Nne ya mwaka wa 2025/2026, huku ajenda zikijadiliwa vizuri ndani ya saa 2 na dakika 09.
Kando ya kikao hiki, Mkurugenzi wa Idara ya Waasisi wa Taifa na Maktaba ya Marais, ndugu Salum A. Kyando, alizungumza na Mwanakawetu hili:
“Sisi pia tunajukumu ya kuhifadhia nyaraka zote za taasisi za umma kama zimefikiwa ukingoni, maana ipo siku inawezekana taasisi hiyo inaweza ikaamuliwa irejeshwe. Kwa hiyo rejea yetu kama taifa ni Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa; hao siyo wengine bali ni sisi.”
Wakati kikao hiki kinamalizika majira ya mchana, hali ya hewa jijini Dodoma ilikuwa ni nyuzi joto 26, unyevunyevu ulikuwa wa asilimia 43, uwezekano wa mvua ulikuwa wa asilimia 5, huku upepo ukivuma kwa kilomita 13 kwa saa.
0717649257














.gif)
Post a Comment