Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila jioni Sara alipanda basi kutoka shule kwenda nyumbani. Alikuwa amekariri ratiba ya mabasi kiasi kwamba hakuwahi kuchelewa.
Siku moja alipofika kituoni alikuta basi limejaa sana. Watu wengi walikuwa wakisubiri lakini kulikuwa na tiketi moja tu iliyobaki.
Kila mtu alitaka kuipata wakati huo Sara alimuona mvulana mdogo akiwa na sare za shule. Alikuwa amechoka na alionekana kuwa na wasiwasi.
Sara akamuuliza "Una shida gani"
Mvulana akasema Mama yangu yuko hospitalini. Nimechelewa kutoka shule na lazima nifike haraka
Sara hakusita akamkabidhi tiketi ile
"Wewe panda mimi nitasubiri basi linalofuata." Mvulana alimshukuru sana na akaondoka.
Dakika ishirini baadaye basi jingine lilifika na Sara akafika nyumbani salama. Alipomweleza mama yake kilichotokea mama yake alimkumbatia na kusema.
Umefanya uamuzi mzuri. Wakati mwingine kutoa nafasi yako kwa anayehitaji zaidi ni kitendo cha ujasiri.
Siku iliyofuata Sara alipofika kituoni alimkuta yule mvulana akisubiri. Alimpa bahasha ndogo iliyokuwa na ujumbe.
"Asante kwa wema wako mama yangu anaendelea vizuri sitaisahau fadhili yako."
Sara alitabasamu aligundua kwamba wema hauhitaji kuwa mkubwa wakati mwingine huanza kwa kuamua kumweka mwingine mbele yako.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment