Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila jambo lilipomtokea alikuwa analia. Akichelewa kupewa chakula analia. Akinyang'anywa toy na mdogo wake analia. Akikosea kufanya kazi ya shule analia tena. Wazazi wake walimfariji kila mara lakini walitamani ajifunze kuwa jasiri na kutafuta suluhisho badala ya kulia kila wakati.
Siku moja akiwa shuleni mwalimu aliwapa wanafunzi kazi ya kuchora. Alipoona penseli yake imevunjika alianza kulia mbele ya darasa. Wenzake walimwangalia kwa mshangao. Mwalimu alimkaribia na kumwambia.
"Kulia si kosa lakini si kila tatizo linatatuliwa kwa machozi. Hebu fikiria unaweza kufanya nini?"
Mtoto alinyamaza kidogo. Mwanafunzi aliyekuwa amekaa karibu naye alimuazima penseli nyingine. Aliendelea kuchora na kumaliza kazi yake vizuri.
Aliporudi nyumbani alikumbuka maneno ya mwalimu. Tangu siku hiyo kila alipokutana na changamoto alianza kujiuliza "Naweza kufanya nini ili kutatua tatizo hili?" Badala ya kulia mara moja alianza kuomba msaada au kutafuta njia ya kulitatua.
Baada ya muda wazazi na walimu wake waliona mabadiliko makubwa. Alikuwa bado analia wakati alipoumia au alipohuzunika sana lakini hakulia tena kwa kila jambo dogo. Alikua mtoto mwenye ujasiri na busara zaidi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment