KOBE NA NJIWA MWEMA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Siku moja kobe alikuwa akitembea polepole kuelekea mtoni kunywa maji. Ghafla aliteleza na kuanguka ndani ya maji. Alijitahidi kuogelea lakini akashindwa kutoka.

Njiwa aliyekuwa juu ya mti alimuona. Haraka akang'oa jani kubwa na kulirusha majini karibu na kobe. Kobe alipanda juu ya jani hilo akafika ufukweni salama.

Baada ya siku chache mwindaji alikuja msituni akitaka kumkamata njiwa. Kobe alipomuona alimng'ata mwindaji mguuni. Mwindaji alishtuka upinde wake ukaanguka chini. Njiwa akaruka juu na kuondoka mazingira hayo.


Njiwa akamshukuru kobe kwa kumsaidia na tangu siku hiyo wakawa marafiki wa karibu.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments