JE! MWANAMKE ANA HAKI YA KUSHIRIKI KUTOA MAAMUZI KATIKA FAMILIA?


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Katika familia moja mume alikuwa akifanya maamuzi yote peke yake bila kumshirikisha mke wake. Aliamua matumizi ya fedha, elimu ya watoto na mipango ya maendeleo bila kushauriana. Hali hiyo ilisababisha migogoro na matatizo ya kifedha. Hata hivyo haki ya kushiriki katika maamuzi ya familia inatambuliwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977, kama ilivyorekebishwa) na pia katika CEDAW (1979) ambavyo vinahimiza usawa na ushirikiano kati ya wanaume na wanawake.

Baadaye walikubaliana kufanya maamuzi kwa pamoja. Walianza kujadili matumizi ya fedha, afya, elimu ya watoto na mipango ya maendeleo. Kwa kufanya hivyo walitekeleza pia misingi ya usawa inayotambuliwa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR, 1948) Ibara ya 1 na 16 zinazosisitiza usawa wa watu wote na haki sawa ndani ya familia.


Kutokana na ushirikiano huo migogoro ilipungua, matumizi ya rasilimali yaliboreshwa, watoto walipata malezi bora na familia ilipata maendeleo. Simulizi hii inaonesha kuwa kushirikisha mwanamke katika maamuzi ya familia huimarisha amani, upendo, ushirikiano na maendeleo jambo linaloungwa mkono na Katiba ya Tanzania (1977) UDHR (1948) na CEDAW (1979).


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872




0/Post a Comment/Comments