Adeladius Makwega – MBAGALA
Agosti 26, 2026, Mwanakwetu alikutana na kundi la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Walikuwa wamechangamka mno. Sehemu kubwa ya kundi hili walipigwa picha, ila mmoja alikuwa anasita kupiga picha.
Mwanakwetu akamuomba ampige picha. Wakati anamshawishi mdau huyu, miongoni mwa maneno yaliyotamkwa na Mwanakwetu yalikuwa haya:
“Ndugu yangu, unaponiona mimi hapa nilipo, ninatembea na ninafanya kazi pahala popote, ninatoka katika kundi fulani la Watanzania. Na wakiniona katika picha, wanasema tumemuona kaka katika mitandao ya kijamii. Wao, ndugu zangu, wanakuwa na furaha, maana mimi ni mali ya kundi fulani la Watanzania.
Popote nilipo, ninaliwakilisha kundi hilo. Kwa hiyo, akija mtu kupiga picha, nikiikwepa picha hiyo, wale ndugu zangu wa Mbagala watakosa uwakilishi. Kwa hiyo, na wewe unalo kundi hilo unaloliwakilisha; liwakilishe vema na usikatae tena kupiga picha.”
Kweli, ndugu yule alikubali kupiga picha.
Je, wewe unayesoma makala haya, unalitambua kundi lako unalotoka? Unaloliwakilisha? Je, unaliwakilisha vema kundi hilo? Siyo katika picha tu, bali katika kila hatua unayopiga katika dunia hii?
Kwa leo inatosha sana.
Hapa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, tunachapa kazi.
Nakutakia siku njema.
0717649257
.gif)




.gif)
Post a Comment