Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kijana mmoja aliishi katika mtaa wa kawaida mjini pamoja na familia yake. Kila siku alikuwa akienda shule akiwa na ndoto kubwa ya kuwa mtu wa kusaidia wengine. Ingawa maisha yao hayakuwa rahisi mama yake alimfundisha kuwa moyo wa upendo na bidii vinaweza kumfikisha mbali.
Siku moja akiwa njiani kurudi nyumbani alimuona mzee mmoja aliyekuwa amekaa pembeni ya barabara akiwa amechoka na hana mtu wa kumsaidia. Watu wengi walipita bila kumjali. Kijana huyo alisimama akamsalimia na kumpa maji aliyokuwa nayo kwenye begi lake.
Mzee huyo alitabasamu na kumwambia “Kitu kidogo ulichofanya leo kinaweza kuwa kikubwa sana kwa mtu mwingine"
Baada ya kufika nyumbani kijana huyo aliandika barua ndogo kwenye karatasi “Usipuuze mtu anayehitaji msaada kwa sababu wema mdogo unaweza kubadilisha siku ya mtu" Aliibandika shuleni.
Wanafunzi wengi waliisoma na kuanza kufanya matendo madogo ya upendo na wengine walijifunza kuheshimu watu wote.
Miaka ilipopita mtaa ule ukawa sehemu yenye watu wenye moyo wa kusaidiana. Kijana huyo alikumbuka kuwa kila kitu kilianza na hatua ndogo tu ya kumjali mtu aliyekuwa amesahaulika.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment