BAHASHA ISIYOKUWA NA JINA


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Siku moja mbele ya ofisi ya shule kulionekana bahasha ya kahawia. Haikuwa na jina wala anuani. Ilikuwa imefungwa vizuri.

Wanafunzi wengi walipoiona walianza kubashiri.

"Labda ina pesa"

"Huenda ni mtihani wa kesho"

"Au ni barua muhimu sana"

Badala ya kuifungua mmoja wa wanafunzi aliichukua na kuipeleka ofisini.

Muda mfupi baadaye mlinzi wa shule aliingia akiwa na wasiwasi. Alikuwa amepewa jukumu la kupeleka bahasha hiyo kwa mkuu wa shule lakini aliidondosha bila kujua.

Mkuu wa shule alipokea bahasha na kusema "Asante kwa kutoipekua mtu mwaminifu hulinda siri na mali ya wengine"


Baadaye ilijulikana kuwa bahasha hiyo haikuwa na pesa wala mitihani. Ndani yake kulikuwa na vyeti vya wanafunzi waliokuwa wamefanya vizuri kwenye mashindano ya mkoa. Kama vingepotea vingechukua muda mrefu kutengenezwa tena.

Siku hiyo wanafunzi walielewa kwamba si kila kitu kinachovutia macho kinapaswa kufunguliwa. Wakati mwingine kuheshimu mali na faragha ya wengine ni jambo la muhimu zaidi.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872

0/Post a Comment/Comments