Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Afya ya watoto ni msingi wa ukuaji na maendeleo ya jamii. Mtoto mwenye afya bora hukua vizuri kimwili, kiakili na kijamii. Ili kuhakikisha watoto wanakuwa na afya njema ni muhimu kuwapatia lishe bora, chanjo, huduma za afya na mazingira safi (World Health Organization [WHO], 2023)
Lishe bora ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto. Watoto wanapaswa kula vyakula vyenye virutubisho kama matunda, mboga, nafaka, maziwa, mayai, samaki na nyama. Lishe duni inaweza kusababisha udumavu, upungufu wa damu na magonjwa mengine (UNICEF, 2023).
Aidha chanjo husaidia kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa hatari kama surua, kifaduro na polio. Pia watoto wanapaswa kuzingatia usafi wa mwili na mazingira kwa kuosha mikono kwa sabuni na kutumia maji safi ili kupunguza maambukizi ya magonjwa (WHO, 2023).
Kwa ujumla afya ya watoto ni jukumu la wazazi, jamii na serikali. Kupitia lishe bora, chanjo, usafi na huduma za afya watoto wanaweza kukua wakiwa na afya njema na kufikia uwezo wao kamili.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment