Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila siku sokoni kulikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa akizunguka kwenye vibanda vya wafanyabiashara. Alikuwa na tabia ya kuiba matunda, pipi na vitu vidogo bila mtu kugundua. Watu walimwita mdokozi mdogo.
Siku moja alijaribu kuiba pochi ya mzee mmoja. Kabla hajakimbia mzee alimshika mkono. Badala ya kumpiga au kumpeleka polisi mzee alimketisha chini na kumuuliza kwa upole "Kwa nini unaiba?"
Mtoto alinyamaza kwa muda kisha akasema "Nina njaa na ninaogopa kurudi nyumbani mikono mitupu."
Mzee alimnunulia chakula na kumpatia kazi ndogo ya kupanga matunda kwenye kibanda chake na akamlipa kwa uaminifu. Kadiri siku zilivyopita mtoto alianza kuona kuwa kufanya kazi kwa bidii kulimpa heshima kuliko kuiba.
Baada ya miezi michache hakuitwa tena mdokozi mdogo. Watu walimjua kama mtoto mchapakazi aliyekuwa tayari kuwasaidia wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment