USIMUHUKUMU MTU BILA USHAIDI

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Jua lilikuwa kali lakini watoto waliendelea kucheza kwenye uwanja wa shule. Kila mmoja alikuwa na furaha isipokuwa mtoto mmoja aliyekaa peke yake chini ya mti. Alionekana mwenye huzuni kwa sababu mpira wa darasa ulikuwa umepotea na wenzake walikuwa wakimshuku kuwa ndiye aliyeuchukua.

Alijaribu kujitetea lakini hakuna aliyemsikiliza.

Muda mfupi baadaye mwalimu alifika na kuwatuliza watoto. Aliwaomba watafute mpira kwa pamoja badala ya kuendelea kulaumiana. Baada ya kutafuta kwa dakika chache walikuta mpira nyuma ya kichaka.

Watoto wote walinyamaza. Waligundua walikuwa wamemhukumu mwenzao bila ushahidi.

Kiongozi wa darasa alimwendea na kusema “Samahani kwa kutokukuamini".

Mtoto huyo alitabasamu na kusema “Nimewasamehe tujifunze kutafuta ukweli kabla ya kumlaumu mtu".

Kuanzia siku hiyo watoto waliahidi kusikilizana, kuheshimiana na kutokutoa hukumu kabla ya kujua ukweli.




emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments