Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kila mtu alimcheka alipobeba kikapu chake kilichokuwa tupu.
Hakuna aliyejua kuwa ndani ya kikapu hicho kulikuwa na ndoto kubwa kuliko
walivyoweza kufikiria.
Kila asubuhi mtoto mmoja alikuwa akienda sokoni akiwa na
kikapu tupu. Watu walimdhihaki wakisema hana kitu cha kuuza.
Baada ya kutoka shuleni alianza kukusanya mbegu za miti ya
matunda kutoka nyumbani na kwa majirani. Alizipanda kwenye vifuko vidogo na
kuzitunza kwa miezi kadhaa. Siku zilivyopita miche hiyo ilikua na kuwa mizuri.
Siku moja alirudi sokoni akiwa na kikapu kilichojaa miche ya maembe, mapapai na machungwa. Watu waliinunua yote kwa sababu walitaka kupanda miti kwenye mashamba yao.
Fedha alizopata alizinunulia vitabu vya shule na vifaa vya
kujifunzia. Baadaye alianza kupanda miti mingi zaidi.
Wale waliokuwa wakimcheka waligundua kuwa mafanikio huanza
na wazo dogo pamoja na uvumilivu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment