Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Saa ilikuwa imekaribia kuanza mtihani. Wanafunzi wote walikuwa tayari isipokuwa mtoto mmoja aliyekuwa akitafuta kalamu yake kwa wasiwasi.
Alipekua begi lake mara nyingi lakini hakuiona. Alitamani kulia kwa sababu alijua hangeweza kufanya mtihani bila kalamu.
Mwanafunzi aliyekuwa amekaa mbele yake aliona hali hiyo. Kimya kimya alimpa kalamu yake ya ziada bila kusema neno lolote. Baada ya mtihani mtoto yule alimshukuru sana. Aliahidi kuwa siku moja angerudisha wema huo.
Miezi kadhaa baadaye mwanafunzi aliyetoa kalamu alifika akiwa amechelewa na alikuwa amesahau daftari lake nyumbani. Bila kusita yule mtoto aliyewahi kusaidiwa alimkopesha daftari lake ili asiadhibiwe na mwalimu.
Mwalimu alitabasamu na kuwaambia wanafunzi wote
"Wema haupotei leo umesaidia mwenzako kesho unaweza kusaidiwa wewe"
Kuanzia siku hiyo wanafunzi wa darasa hilo walijenga utamaduni wa kusaidiana badala ya kuchekana au kubezana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment