UNICEF YAONGEZA JITIHADA KUBORESHA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO TANZANIA

 

Mwanakwetukids

 Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania limeendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha watoto wote wanapata usajili wa vizazi mara baada ya kuzaliwa ikiwa ni hatua muhimu ya kuwapatia utambulisho wa kisheria na haki zao za msingi yamesemwa hayo jijini Dar es Salaam tarehe 2/07/2026

Mpango huo unalenga kupunguza idadi ya watoto wasioandikishwa nchini jambo ambalo limekuwa changamoto katika baadhi ya maeneo ya vijijini na mijini ambapo baadhi ya watoto hukosa huduma muhimu kama elimu, afya na ulinzi wa kijamii kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa za UNICEF usajili wa vizazi unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha watoto wanatambulika rasmi na serikali jambo linalosaidia kupanga na kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa jamii nzima.

Serikali kupitia taasisi husika imeahidi kuendelea kushirikiana na UNICEF na wadau wengine ili kuboresha mifumo ya usajili wa vizazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa, pamoja na kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi hasa maeneo ya pembezoni.

Aidha wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kusajiliwa mapema mara baada ya kuzaliwa ili kuwapa haki ya msingi ya utambulisho rasmi.




emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments