Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Harufu ya maandazi yaliyokuwa yanatoka jikoni ilitosha kumfanya ashindwe kuvumilia. Tumbo lilianza kuguruma macho yakatafuta sahani iliyokuwa imefunikwa mezani. Hakukuwa na mtu aliyekuwa akimwangalia. Hiyo ilionekana kuwa nafasi yake.
Kwa hatua za polepole aliingia jikoni akafunua sahani na kuchukua andazi kubwa. Bila kusubiri akaliuma kwa pupa.
Sekunde chache baadaye uso wake ukabadilika. Mdomo ulianza kuwaka moto machozi yakaanza kumtoka na akakimbilia kunywa maji. Kumbe andazi lile lilikuwa limejazwa pilipili kali na lilikuwa limeandaliwa kwa ajili ya mtu aliyependa pilipili.
Wazazi walipofika hawakumfokea. Walimweleza kuwa kama angesubiri na kula pamoja na wengine usingepata adhabu hiyo ya kujitakia.
Tangu siku hiyo aliacha tabia ya uroho na kujifunza kuwa subira na kushiriki ni tabia zinazomfanya mtoto aheshimiwe.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment