SHUJAA WA KWELI SI YULE ANAYESHINDA MCHEZO PEKEE BALI ANAWASAIDIA WENGINE

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

"Kicheko kilikuwa kikitawala uwanja lakini ghafla sauti ya kilio kidogo ilifanya kila kitu kionekane kimya..."

Jioni ile watoto walikuwa wakikimbizana kwa furaha baada ya kutoka shule. Mipira iliruka, vicheko vilisikika kila kona na kila mmoja alifurahia mchezo.

Lakini pembeni ya uwanja chini ya mti mkubwa alikuwapo mtoto mmoja aliyekaa peke yake. Alikuwa ameinamisha kichwa huku machozi yakimdondoka taratibu.

Asha alipomuona alisimama ghafla. Aliwaacha marafiki zake na kumfuata.

"Mbona unalia?" aliuliza kwa sauti ya upole.

Mtoto huyo alifuta machozi na kusema "Nimepoteza begi langu la shule naogopa kurudi nyumbani bila hilo.

Bila kusita Asha aliwaomba marafiki zake waache mchezo kwa muda. Wote waliinuka na kuanza kulitafuta begi hilo. Baada ya kulitafuta kwa muda waliliona limeegeshwa karibu na uzio wa uwanja.

Mtoto huyo alipolipokea begi lake uso wake ulijaa tabasamu. Aliwashukuru kwa moyo wote.

Kuanzia siku hiyo watoto wa eneo hilo walijifunza kwamba kusaidia mwenye shida ni muhimu kuliko kuendelea kucheza huku ukipuuza kilio cha mwenzako.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments