Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Serikali ya Tanzania imeeleza mpango wake wa kuanzisha mfumo maalum wa Child SIM Card unaolenga kuwalinda watoto dhidi ya maudhui hatarishi na unyanyasaji wa mtandaoni ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usalama wa watoto katika matumizi ya teknolojia.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2026/27 Waziri Dkt. Dorothy Gwajima alisema serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) po katika hatua za mazungumzo ya utekelezaji wa mpango huo.
Dkt. Gwajima alisema ongezeko la matumizi ya simu janja na intaneti miongoni mwa watoto limeongeza hatari ya kufikiwa kwa maudhui yasiyofaa hivyo serikali inalenga kuweka mfumo utakaosaidia kuchuja na kudhibiti maudhui hayo moja kwa moja kupitia mtandao.
Kwa mujibu wa waziri huyo mfumo huo wa Child SIM Card unatarajiwa kusaidia kuhakikisha watoto wanapata mazingira salama ya kidijitali yanayowawezesha kutumia teknolojia kwa ajili ya elimu na mawasiliano bila kuathiriwa na maudhui hatarishi.
Aidha serikali imeeleza kuwa mpango huo utahusisha pia uhamasishaji kwa wazazi na walezi kuhusu usimamizi wa matumizi ya intaneti kwa watoto pamoja na kuimarisha elimu ya usalama wa mtandaoni katika jamii.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment