MTOTO ALIYEAMINI KESHO ITAKUA BORA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Asubuhi ya Jumatatu mwalimu aliwaambia wanafunzi wote watoe daftari la kazi ya nyumbani. Kila mmoja alitoa isipokuwa mtoto mmoja aliyekuwa ameinamisha kichwa.

"Huna daftari?" mwalimu aliuliza kwa upole.

Mtoto huyo akajibu kwa sauti ya chini "Nilikuwa na daftari moja tu. Liliisha jana na nyumbani hatukuwa na fedha za kuninunulia jingine."

Darasa likatulia. Mwanafunzi mmoja akainua mkono na kusema "Mwalimu nina madaftari mawili mapya. Naweza kumpa moja."

Baada ya kuona hivyo wanafunzi wengine wakachangia kalamu na vifaa vingine vya shule walivyokuwa navyo.

Siku iliyofuata mtoto huyo alifika shuleni akiwa na tabasamu kubwa. Alifanya kazi zote kwa bidii na baadaye akawa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri darasani.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments