Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Asubuhi moja mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu. Watoto walikuwa wakikimbilia madarasani huku wakijikinga na mifuko yao. Neema mwanafunzi wa darasa la tano alifika shuleni akiwa hajala chochote nyumbani kwa sababu mama yake alikuwa ameondoka mapema kutafuta kazi za vibarua.
Wakati wa mapumziko alikaa kimya chini ya mti akitazama wenzake wakila. Rafiki yake Asha aligundua hali hiyo. Bila kusema mengi alimkaribia na kusema "Tule pamoja" Akamgawia nusu ya uji na maandazi aliyokuwa amebeba.
Neema alikataa mwanzoni kwa aibu lakini Asha alimwambia "Leo nimekusaidia mimi kesho unaweza kumsaidia mwingine.
Miaka michache baadaye Neema alipata ufadhili wa masomo kutokana na juhudi zake darasani. Hakuwahi kusahau wema aliotendewa. Alipoanza kufanya kazi alianzisha utaratibu wa kuchangia kifungua kinywa kwa wanafunzi wenye uhitaji katika shule yake ya zamani.
Asha alipomtembelea siku moja alikuta watoto wengi wakifurahia uji wa asubuhi. Neema akatabasamu na kusema "Kikombe kile ulinichogawia kilinifundisha kuwa msaada mdogo unaweza kubadili maisha ya mtu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment