MOYO WA HURUMA HAUPIMWI KWA MEDALI

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids 

Siku ya mashindano ya riadha shuleni ilifika. Watoto wote walikuwa na furaha wakijiandaa kukimbia. Kabla ya mbio kuanza mtoto mmoja aligundua kuwa kiatu cha rafiki yake kilikuwa kimechanika.

Badala ya kumcheka alimvua kiatu chake kizima na kumpa rafiki yake akivae huku yeye akivaa kile kilichokuwa kizima upande mwingine. Walikimbia mbio wakiwa na viatu tofauti.

Ingawa hawakushinda nafasi ya kwanza walipomaliza mbio walipigiwa makofi na walimu pamoja na wanafunzi wote. Mwalimu alisema Mshindi wa kweli si anayefika wa kwanza pekee bali anayejali wengine.

Watoto wote walijifunza kuwa urafiki huruma na kusaidiana vina thamani kubwa kuliko medali.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments