MCHELE WA MWISHO

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Jioni moja mama alipofungua debe la mchele aligundua umebaki kikombe kimoja tu. Baba alikuwa bado hajarudi kazini na hakukuwa na pesa za kununua chakula kingine.

Watoto walipoona hali hiyo hawakulalamika. Mtoto mkubwa akasema "Mama pika huo mchele Tutaugawana wote."

Mama alipika wali na kuugawa kwa usawa. Kila mmoja alipata kiasi kidogo lakini hakuna aliyenung'unika.

Wakati familia ikianza kula mlango uligongwa. Alikuwa jirani aliyekuwa amekuja kumrudishia baba deni alilokuwa amekopa wiki kadhaa zilizopita.

Baba alipofika muda mfupi baadaye alifurahi kuona familia yote ilivumilia hali ngumu kwa upendo na umoja. Kesho yake waliinunua chakula cha kutosha.

Mama aliwaambia watoto wake "Familia yenye upendo haipimwi kwa wingi wa chakula mezani bali kwa jinsi inavyoshirikiana wakati wa shida".

Watoto walitabasamu.wakijua kwamba walikuwa wamejifunza somo ambalo hawangesahau kamwe.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments