Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Jioni moja nyumbani mama alikuwa akiandaa chakula huku watoto wakimsaidia kazi ndogo ndogo. Mtoto mmoja alijitolea kubeba sahani kwenda mezani.
Alipokuwa akitembea mguu wake uliteleza. Sahani ikaanguka na kuvunjika vipande vipande.
Kwa hofu alisimama kimya. Alijua sahani hiyo ilikuwa mojawapo ya sahani ambazo mama alipenda sana. Alitarajia kufokewa vikali.
Mama alifika pale akaangalia vipande vya sahani kisha akamuuliza kwa upole "Umeumia"?
Mtoto alitikisa kichwa. Mama akasema Muhimu ni kwamba uko salama sahani inaweza kununuliwa nyingine.
Maneno hayo yalimfariji sana. Badala ya kujificha au kusema uongo alikiri kosa lake na kusaidia kusafisha vipande vya sahani.
Tangu siku hiyo alijifunza kuwa kusema ukweli ni bora kuliko kuficha makosa. Naye mama alifurahi kuona mtoto wake anakuwa mwaminifu na mwenye kuwajibika.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment