Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mtoto aliyependa kucheza kuliko kufanya kazi za nyumbani. Kila alipomaliza shule, alikimbilia uwanjani na kuacha majukumu yake.
Siku moja bibi yake alimpa mbegu moja ndogo na kusema "Iweke ardhini imwagilie maji kila siku halafu uwe na subira."
Mtoto alifanya hivyo kwa siku mbili tu. Alipoona hakuna kilichotokea akaacha kuimwagilia. Baada ya wiki moja alikuta mbegu imekauka.
Bibi akampa mbegu nyingine. Safari hii mtoto aliamua kutokata tamaa. Kila asubuhi aliimwagilia maji na kuiondoa magugu yaliyokuwa karibu nayo. Alifanya hivyo kwa wiki nyingi.
Siku moja chipukizi la kijani likachomoza ardhini. Kadiri siku zilivyopita likawa mmea mzuri uliojaa majani. Baadaye ulitoa maua na matunda.
Mtoto alitabasamu na kusema "Sasa nimeelewa vitu vizuri haviji kwa haraka. Vinahitaji muda, juhudi na subira".
Kuanzia siku hiyo hakukimbia tena majukumu yake. Alijifunza kuwa mafanikio huanza na hatua ndogo zinazorudiwa kila siku.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment