Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na mashindano ya mpira wa miguu kati ya shule mbili za msingi. Dakika zilikuwa zimebaki chache na timu ya shule ya Kijani ilikuwa nyuma kwa bao moja.
Wachezaji wengi walitaka kufunga peke yao ili wasifiwe. Walikuwa hawapeani pasi vizuri jambo lililowafanya wapoteze nafasi nyingi.
Nahodha wa timu aliwaita wenzake haraka na kusema "Tusicheze kwa ajili ya sifa. Tucheze kama timu".
Mchezo ulipoanza tena kila mchezaji alianza kumpasia mwenzake. Dakika ya mwisho mpira ulimfikia mtoto ambaye hakuwa amewahi kufunga bao msimu mzima. Badala ya kuogopa alipiga shuti la nguvu.
Gooooo! Mpira uliingia wavuni. Mashabiki walishangilia kwa nguvu.
Dakika chache baadaye filimbi ya mwisho ililia. Mchezo uliisha kwa sare ingawa hawakushinda. Walimu na wazazi waliwapongeza kwa ushirikiano wao na mchezo wa kiungwana.
Kocha aliwaambia "Leo mmejifunza somo kubwa kuliko ushindi. Timu yenye umoja inaweza kufanya mambo makubwa".
Kuanzia siku hiyo wachezaji waliacha kugombania umaarufu na wakaanza kucheza kwa kushirikiana. Msimu uliofuata walitwaa ubingwa wa wilaya.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872

Post a Comment