Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu siku ile matokeo ya mitihani yalipotolewa. Mtoto mmoja alitembea polepole akielekea nyumbani akiwa ameshika karatasi ya matokeo. Alikuwa amepata alama za chini kuliko alivyotarajia.
Alipofika nyumbani aliogopa kumwonesha mama yake matokeo hayo. Alidhani angefokewa au kuadhibiwa. Lakini mama yake alimtazama kwa upole na kusema "Alama si mwisho wa maisha tuangalie tulikosea wapi.
Kuanzia siku hiyo mama alianza kukaa naye kila jioni wakisoma pamoja. Walizima televisheni mapema wakatenga muda wa kufanya mazoezi ya masomo na kila mwisho wa wiki walipitia makosa aliyokuwa amefanya darasani.
Baada ya miezi kadhaa mitihani iliyofuata ilifika. Safari hii alifaulu vizuri zaidi kuliko mara ya kwanza. Hakushika nafasi ya kwanza lakini aliongeza alama nyingi na walimu wake waliona mabadiliko makubwa.
Aliporudi nyumbani na matokeo mapya mama yake alitabasamu na kusema "Nimefurahia juhudi zako kuliko alama zako".
Mtoto aligundua kuwa mafanikio hayaji kwa bahati bali kwa kujifunza kutokana na makosa na kutokata tamaa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment