Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku ya kwanza ya muhula mpya mwalimu aliingia darasani akiwa amebeba sanduku la mbao lililofungwa. Aliliweka mezani na kusema.
"Ndani ya sanduku hili kuna kitu kitakachobadili maisha ya mmoja wenu".
Watoto wote walijawa na hamu. Kila siku walijiuliza sanduku hilo lina nini.
Baada ya wiki moja mwalimu aliwaita wanafunzi mmoja baada ya mwingine walitazame ndani ya sanduku lakini akawakataza wasimwambie yeyote walichoona.
Kila mtoto alipotoka alikuwa anatabasamu.
Hatimaye ilifika zamu ya mtoto aliyekuwa akijiona hafai kwa sababu alifanya vibaya darasani. Alifungua sanduku taratibu.
Ndani hakukuwa na zawadi wala pesa kulikuwa na kioo.
Chini ya kioo kulikuwa na ujumbe uliosomeka.
"Huyu ndiye mtu mwenye uwezo wa kubadili maisha yako anza kwa kujiamini"
Mtoto huyo alitoka akiwa na tabasamu. Kuanzia siku hiyo alianza kusoma kwa bidii, kuuliza maswali darasani na kutokata tamaa.
Mwishoni mwa mwaka alifanya vizuri kuliko alivyowahi kufanya. Wanafunzi walipojua siri ya sanduku walielewa kwamba mafanikio huanza kwa kuamini uwezo wako mwenyewe.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment