Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.com
Kila siku fedha za kununua vitabu vya maktaba zilikuwa zikipotea darasani. Wanafunzi wengi walianza kutuhumiana na hali hiyo ilileta ugomvi kati yao.
Siku moja mwalimu aliwaomba wanafunzi wote wakae kwa utulivu na kueleza ukweli bila kuogopa. Baada ya ukimya wa muda mfupi mtoto mmoja alisimama na kukiri kuwa ndiye aliyekuwa akichukua fedha hizo. Alisema hakuzitumia kwa starehe bali alinunua chakula kwa mdogo wake ambaye mara nyingi alilala njaa nyumbani.
Mwalimu hakumdhalilisha mbele ya wenzake. Badala yake aliwasiliana na wazazi wake na viongozi wa kijiji ili familia hiyo ipate msaada. Wanafunzi walikusanya vifaa vya shule na chakula ili kuwasaidia.
Tangu siku hiyo mtoto huyo alibadilika akawa mfano wa uaminifu na bidii darasani. Wanafunzi pia walijifunza kuwa ni muhimu kutafuta ukweli kabla ya kumhukumu mtu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment