AJIRA HAIKUMTAFUTA ALIUNDA FURSA YAKE MWENYEWE

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.com 

Baada ya kumaliza kidato cha nne kijana mmoja alitamani kuendelea na masomo lakini hali ya kifedha ya familia haikuruhusu. Badala ya kukaa nyumbani akilalamika aliamua kutumia ujuzi mdogo aliokuwa nao kuanza kujiajiri.

Alikopa fedha kidogo kutoka kwa mjomba wake na kuanzisha biashara ya kuuza matunda sokoni. Mwanzoni biashara ilikuwa ngumu baadhi ya siku aliuza kidogo sana na wengine walimdharau wakisema elimu yake imepotea bure. Hata hivyo hakukata tamaa.

Kwa bidii na nidhamu biashara yake ilianza kukua. Baada ya mwaka mmoja alifungua kibanda kikubwa akaongeza bidhaa nyingine na baadaye akaajiri vijana wawili wa mtaani. Aliendelea kujifunza mbinu za biashara kupitia vitabu na mafunzo ya mtandaoni.

Leo hii anaendesha duka lenye mafanikio na anawasaidia wazazi wake pamoja na kulipia ada ya mdogo wake. Mara nyingi huwaambia vijana wenzake kwamba elimu ni msingi muhimu lakini mafanikio yanahitaji pia ubunifu, juhudi na uthubutu wa kuanza.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments