WATOTO 4,000 WAHITAJI UPASUAJI WA MOYO NCHINI

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.

Zaidi ya watoto 4,000 nchini Tanzania wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo kutokana na matatizo mbalimbali ya moyo yanayowakabili huku wataalamu wa afya wakitoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto hospitalini mapema pindi wanapoonyesha dalili za ugonjwa huo.

Taarifa hiyo ilitolewa na viongozi wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) wakati wa hafla ya kupokea msaada wa shilingi milioni 20 kutoka KCB Bank Tanzania kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 26 Juni 2026.

Viongozi wa JKCI walieleza kuwa watoto wengi huzaliwa na matatizo ya moyo au hupata magonjwa ya moyo wanapokuwa wakikua. Walibainisha kuwa matibabu ya mapema yanaongeza nafasi ya mtoto kupona na kuendelea na maisha ya kawaida.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo fedha zilizotolewa zitatumika kugharamia vipimo, matibabu na upasuaji kwa baadhi ya watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wa kumudu gharama hizo.

Aidha JKCI imeendelea kuimarisha huduma za kibingwa za upasuaji wa moyo nchini ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolazimika kutafuta matibabu nje ya Tanzania. Wazazi na walezi wametakiwa kuwahi hospitalini mara wanapoona dalili kama mtoto kuchoka haraka kupumua kwa shida, kubadilika rangi ya midomo kuwa ya samawati au kushindwa kunyonya vizuri kwa watoto wachanga.


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments