THAMANI YA MTU HAIPIMWI KWA MAVAZI

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.com 

Kulikua na mvulana wa darasa la sita aliyependa sana kusoma. Kila siku alitembea zaidi ya kilomita mbili kwenda shuleni. Tatizo pekee lilikuwa kwamba viatu vyake vilikuwa vimechakaa sana.

Wanafunzi wengine walimcheka. "Angalia viatu vyake!" walisema huku wakicheka.

 Hakujibu aliendelea kusoma kwa bidii na kuheshimu kila mtu.

Siku moja mwalimu alitangaza mashindano ya sayansi. Kila mwanafunzi alitakiwa kuleta wazo la kutatua tatizo la kijijini.

Wengi walileta michoro mizuri lakini yeye alileta kifaa rahisi alichotengeneza kwa kutumia chupa za plastiki zilizotupwa. Kifaa hicho kilisaidia kukusanya maji ya mvua kwa matumizi ya bustani za shule.

Majaji walivutiwa sana. Wazo lake lilikuwa rahisi na gharama nafuu na lenye manufaa kwa jamii alishinda mashindano.Siku ya kutoa tuzo mkuu wa shule alisema.


"Watu wengi waliona viatu vyake chakavu wachache waliona akili yake"

Ukumbi mzima ulitulia wanafunzi waliomcheka waliona aibu.

Baada ya hapo shule ilimsaidia kupata sare na viatu vipya. Lakini kilichomfurahisha zaidi si viatu hivyo ilikuwa heshima aliyopata kutokana na juhudi zake.

Miaka kadhaa baadaye alikua mhandisi aliyebuni miradi ya kusaidia vijiji kupata maji safi.

Alipoulizwa siri ya mafanikio yake alisema.

"Usikubali watu wakufafanue kwa kile ulicho nacho. Waoneshe wewe ni nani kupitia kile unachoweza kufanya".


emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872






0/Post a Comment/Comments