SUNGURA NA KASA

 


Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.

Kulikuwa na sungura aliyekuwa anajivunia kasi yake ya kukimbia. Kila siku aliwacheka wanyama wengine hasa kasa kwa sababu alikuwa akitembea polepole sana.

Siku moja sungura alimwambia kasa “Wewe ni mnyama wa polepole zaidi niliyewahi kuona!”

Kasa alitabasamu na kujibu “Ni kweli mimi ni wa polepole lakini ninaweza kufika ninapokwenda ikiwa sitaacha kutembea".

Sungura alicheka sana. Wanyama wengine walipendekeza washindane mbio ili waone nani angefika mwisho wa njia kwanza.

Mbio zilipoanza sungura alikimbia kwa kasi kubwa na kumuacha kasa mbali nyuma. Alipoona amemtangulia sana aliamua kupumzika chini ya mti.

“Nitalala kidogo tu” alisema. Lakini usingizi ulimchukua. Wakati huo kasa aliendelea kutembea taratibu bila kusimama. Hatimaye alimkaribia sungura aliyekuwa amelala na akampita.

Sungura alipoamka alikimbia kwa nguvu zote kuelekea mwisho wa njia. Lakini ilikuwa imechelewa. Kasa alikuwa tayari amefika na kushinda mbio.

Wanyama wote walimshangilia kasa. Sungura alijifunza somo muhimu siku hiyo.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872


0/Post a Comment/Comments