Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids.
Serikali imeendelea kusisitiza juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini kwa kushirikiana na wazazi, walezi, walimu na wadau wa ustawi wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto anakua katika mazingira salama.
Akizungumza tarehe 26 Juni 2026 jijini Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu alisema kuwa bado kuna changamoto za ukatili wa kimwili, kingono, kisaikolojia na kutelekezwa kwa watoto katika baadhi ya maeneo nchini. Alisema vitendo hivyo vinakiuka haki za mtoto na vinaathiri maendeleo yake kielimu, kiafya na kijamii.
Waziri huyo alieleza kuwa Serikali imeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za mtoto, kuimarisha dawati za jinsia na watoto katika vituo vya polisi pamoja na kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa ili kubaini na kushughulikia matukio ya ukatili mapema.
Aidha wataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa malezi kwa kuwapa watoto ulinzi, elimu, huduma za afya na maadili mema. Pia aliwahimiza wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanaposhuhudia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili hatua za kisheria zichukuliwe haraka.
Wadau wa haki za watoto walieleza kuwa ushirikiano wa jamii nzima ni muhimu katika kutokomeza ukatili na kuhakikisha watoto wanapata fursa ya kukua, kujifunza na kufikia ndoto zao katika mazingira salam.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872




Post a Comment