SAUTI ILIYOTOKA GIZANI

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids.

Usiku mmoja Rehema na kaka yake Musa walikuwa nyumbani na bibi yao wakati mvua kubwa ilinyesha. Umeme ukakatika na nyumba ikawa kimya kabisa.

Ghafla wakasikia sauti nje ya mlango

"Hodi.. hodi... naomba msaada". Rehema akaogopa na kujificha nyuma ya bibi. Musa alitaka kufungua mlango haraka lakini bibi akamzuia.

"Kwanza tuulize ni nani" alisema bibi kwa utulivu.

Musa akauliza ni nani?"

Sauti ikajibu "Mimi ni mzee Juma. Baiskeli yangu imeharibika na mvua imenyesha sana. Naomba nijifiche kidogo."Bibi akachungulia dirishani na kumwona kweli ni jirani yao mzee Juma akiwa amelowana kabisa.


Wakamfungulia mlango wakampa taulo la kujifuta na kikombe cha chai ya moto. Baada ya mvua kupungua mzee Juma aliwashukuru sana na kurudi nyumbani salama.

Rehema akamuuliza bibi yake Kwa nini hukuufungua mlango mara moja?"

Bibi akatabasamu akasema ni vizuri kuwasaidia watu lakini ni muhimu pia kuhakikisha usalama wetu kwanza".

Kuanzia siku hiyo Rehema na Musa walijifunza kuwa ujasiri unaenda sambamba na busara.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872




0/Post a Comment/Comments