RAFIKI WA KWELI HUONEKANA WAKATI WA SHIDA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Hapo zamani za kale kulikuwa na sungura mdogo aliyeitwa Tunu. Tunu alipenda kucheza siku nzima lakini hakupenda kuwasaidia wenzake.

Siku moja alipokuwa akicheza msituni aliteleza na kuanguka kwenye shimo. Alijaribu kutoka lakini hakufaulu. Akaanza kuita kwa sauti.

"Naomba msaada! Naomba msaada!"

Njiwa mmoja aliyekuwa anaruka juu alisikia kilio chake. Aliwaita marafiki zake kwa pamoja wakashusha mzabibu mrefu ndani ya shimo. Tunu akaupanda na kutoka salama.

Tunu aliwashukuru sana njiwa. Aligundua kuwa kusaidiana ni jambo muhimu tangu siku hiyo alianza kuwasaidia wanyama wote waliokuwa na shida.

Wanyama wa msituni wakampenda zaidi kwa sababu alikuwa mkarimu na mwenye moyo wa kusaidia.

emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872





0/Post a Comment/Comments