Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Siku moja mtoto alikuwa akitoka shuleni kuelekea nyumbani. Anga lilikuwa na mawingu mazito lakini hakudhani mvua ingenyesha.
Alipokuwa njiani pamoja na marafiki zake upepo mkali ulianza kuvuma. Dakika chache baadaye mvua kubwa ilianza kunyesha.
Watoto wengi walikimbia kutafuta mahali pa kujikinga.Alikimbilia kwenye kibanda kidogo cha mfanyabiashara mmoja wa matunda. Humo alikuta watu wengine wakisubiri mvua ipungue.
Baada ya muda aliona mama mmoja akiwa na mtoto mdogo mgongoni. Walikuwa wamelowa sana kwa sababu hawakuwa na mwavuli. Mtoto yule alikuwa na koti lake kwenye begi.
Bila kusita alimpa mama huyo koti hilo ili amlinde mtoto dhidi ya mvua.
"Asante sana mwanangu" alisema mama huyo kwa furaha.
Mvua ilipopungua kila mtu aliendelea na safari yake. Baraka alifika nyumbani akiwa amelowa kidogo lakini alijisikia furaha kwa sababu alikuwa amemsaidia mtu aliyekuwa na uhitaji mkubwa zaidi.
Jioni hiyo alipowaeleza wazazi wake kilichotokea walimpongeza kwa kuwa na moyo wa huruma na kusaidia wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment