MSEMA UONGO AKISEMA KWELI HAAMINIKI

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids.com

Katika mji mmoja kulikuwa na mtoto aliyependa kufanya mzaha. Mara nyingi alipokuwa akicheza na watoto wenzake aliwaambia mambo ambayo hayakuwa ya kweli ili kuwachekesha au kuwashangaza.

Siku moja aliwaambia watoto kwamba kulikuwa na nyoka mkubwa karibu na uwanja wa michezo. Watoto wote wakakimbia kwa hofu. Baadaye waligundua kwamba hakukuwa na nyoka yeyote. Mtoto huyo akacheka sana.

Baada ya muda alifanya hivyo tena. Aliwaambia watu kuwa kulikuwa na moto katika nyumba moja karibu na mtaa wao. Majirani walikimbia kwenda kusaidia lakini walipofika walikuta hakuna moto. Watu walikasirika na kuondoka.

Siku kadhaa baadaye alipokuwa akitembea mitaani aliona moshi ukitoka katika nyumba moja. Moto ulikuwa umeanza kweli. Akaanza kupiga kelele.

"Moto! Moto! Njooni msaidie!"

Lakini watu wengi hawakumjali. Walidhani alikuwa anatania kama siku zilizopita. Ilikuwa mpaka watu wachache walipoona moshi kwa macho yao ndipo walipokuja kusaidia.

Baada ya tukio hilo mtoto huyo alitambua kuwa kusema uongo kulikuwa kumefanya watu wasimwamini. Akaamua kuacha kusema uongo na kuanza kusema ukweli kila wakati.

Tangu siku hiyo watu waliona mabadiliko yake na polepole wakaanza kumwamini tena.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments