KUKUBALI MAKOSA NI HATUA YA KWANZA YAKUA BORA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids.com

Kulikuwa na mtoto aliyekuwa akisoma shule ya msingi. Siku moja alisahau kufanya kazi ya nyumbani aliyopewa na mwalimu.

Alipoingia darasani mwalimu aliwaomba wanafunzi wakabidhi madaftari yao. Mtoto huyo akaogopa na kusema."Daftari langu lilichukuliwa na upepo njiani."

Mwalimu hakusema chochote lakini alimpa nafasi nyingine ya kuleta kazi yake kesho.

Kesho yake alisahau tena kufanya kazi hiyo. Safari hii akasema

"Nilikuwa mgonjwa sana jana usiku ndiyo maana sikuweza kuandika."

Lakini baadhi ya wanafunzi walijua alikuwa akicheza muda mwingi badala ya kusoma.

Siku chache baadaye kulikuwa na shindano la darasani. Mtoto huyo alijitahidi sana na akapata alama nzuri. Alipomwambia mwalimu kwamba alikuwa amesoma kwa bidii mwalimu alifurahi lakini akamwambia "Mafanikio yako ni mazuri lakini watu huamini zaidi maneno ya mtu anayekuwa mkweli kila wakati."

Mtoto huyo alitafakari maneno hayo. Akaamua kuacha kutoa visingizio na kuanza kuwajibika kwa makosa yake.

Tangu siku hiyo alipokosea alikubali na alipopewa kazi aliifanya kwa wakati. Polepole walimu na wanafunzi wenzake wakaanza kumheshimu zaidi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments