KILA MTOTO ANA HADITHI YA MAFANIKIO INAYOSUBIRI KUANDIKWA

 

Emakulata Msafiri 

Mwanakwetukids

Watoto ni sehemu muhimu ya jamii lakini mara nyingi sauti zao husahaulika au kupuuzwa. Kila mtoto ana mawazo, hisia na ndoto ambazo zinapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa. Kuwapa watoto nafasi ya kujieleza huwasaidia kujenga kujiamini na kukuza uwezo wao wa kufikiri.

Katika familia wazazi na walezi wanapaswa kuwasikiliza watoto wanapozungumza kuhusu changamoto, mahitaji na matarajio yao. Mtoto anayesikilizwa hujihisi kuwa wa thamani na hupata ujasiri wa kushiriki mawazo yake bila hofu. Hali hii huimarisha uhusiano mzuri kati ya mtoto na wazazi wake.

Shuleni walimu wanapaswa kuwahimiza wanafunzi kushiriki katika mijadala na shughuli mbalimbali zinazowapa nafasi ya kutoa maoni yao. Watoto wanapohusishwa katika maamuzi yanayowahusu kujifunza kuwajibika na kuheshimu maoni ya wengine.

Jamii nayo ina wajibu wa kulinda haki za watoto na kuhakikisha wanapata fursa sawa za maendeleo. Kusikiliza sauti za watoto ni njia mojawapo ya kutambua changamoto wanazokutana nazo na kutafuta suluhisho zinazofaa.

Kwa kumalizia kusikiliza sauti ya mtoto si ishara ya udhaifu bali ni hatua muhimu ya kujenga kizazi chenye kujiamini, maarifa na uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii. Mtoto akisikilizwa leo atakuwa raia bora wa kesho.

emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872



0/Post a Comment/Comments